Waarabu wa Saudia kumrudisha De Gea kwenye soka
Eric Buyanza
July 8, 2024
Share :
Kipa wa zamani wa Manchester United, David De Gea, yuko kwenye mazungumzo na vilabu viwili vya Saudi Arabia, mazungumzo yanayoweza kumrudisha mkongwe huyo kwenye soka.
David mwenye umri wa miaka 33 tayari amefanya mazungumzo na klabu ya Al-Shabab na nyingine moja ambayo haikutajwa.
De Gea amekuwa hana timu tangu amalize mkataba wake na United mwishoni mwa 2022/2023.