Waarabu wachuana kuinasa saini ya Bruno Fernandes
Eric Buyanza
July 6, 2024
Share :
Manchester United imempa kiungo Bruno Fernandes, ruhusa ya kuanza mazungumzo na klabu za Saudi Arabia, huku klabu mbili za nchi hiyo zikisemekana kuchuana katika kuinasa saini yake.
Teamtalk wameripoti kuwa klabu hizo mbili zinazomtaka kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 29 ni Al Nassr na Al Ittihad.