Waarabu wafikia bei kwa kiungo wa Man City
Sisti Herman
August 13, 2026
Share :

Klabu ya Al Qadsiah wamefikia makubaliano na Manchester City kuhusu uhamisho wa kiungo Tijjani Reijnders kwa ada ya €61M.
Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, makubaliano kati ya klabu hizo mbili yamekamilika na Man City wako tayari kumuuza; sasa dili hilo linategemea uamuzi wa mchezaji mwenyewe kuhusu kwenda Saudi Arabia.
Endapo Reijnders atakubali, Al Qadsiah wako tayari kukamilisha dili hilo kwa haraka na Manchester City Reijnders alikuwa pia akipokea ofa kutoka Nottingham Forest, huku Newcastle wakijiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.





