Waarabu wamwaga kuwakutania AJ na Francis
Sisti Herman
January 7, 2024
Share :
Rasmi sasa pambano la bondia wa uzito wa juu wa kiingereza Anthony Joshua na bingwa wa zamani wa MMA aliyegeukia kwenye masumbwi Francis Nganou limethibitika kuwepo kupigwa tarehe 9 ya mwezi machi mjini Riyadh, nchini Saudi Arabia.
Hili litakuwa ni pambano la pili kwa Francis Nganou tangu alipoamua kuingia kwenye ngumi za kulipwa akitoka kwenye Sanaa ya mapigano mchanganyika (MMA). Pambano lake la kwanza lilikuwa ni DHIDI ya Tyson Fury ambapo ulishangaza uliwengu kwa kiwango Bora Sana.