pmbet

Waasi wa Houthi waimbia Israel, tutalipiza kisasi kikubwa

Eric Buyanza

July 22, 2024
Share :

Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wameahidi kulipiza kisasi dhidi ya shambulizi kali la Israel kwenye bandari yao ya Hodeidah. 

Shambulizi la Israel nchini Yemen, lilisababisha moto kwenye tanki za mafuta katika bandari hiyo muhimu na lilijiri siku moja baada ya shambulio baya lililofanywa na Wahouthi nchini Israel. 

DW imeripoti kuwa jana Jumapili, Israel ililiharibu kombora lililorushwa kutokea Yemen na kuyashambulia maeneo ya kusini mwa Lebanon. Wakaazi wa kusini mwa Gaza waliripoti kutokea kwa mapigano katika eneo la Rafah. 

Msemaji wa kijeshi wa Wahouthi Yahya Saree alisema jibu la waasi hao kwa uchokozi wa Israel dhidi ya nchi yao haliepukiki na litakuwa kubwa zaidi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet