pmbet

Waasi wa M23 waiteka miji miwili nchini Kongo

Eric Buyanza

July 1, 2024
Share :

Baada ya waasi wa M23 kuiteka miji midogo miwili muhimu katika wilaya ya Lubero mkoani Kivu ya Kaskazini, waasi hao wanaonekana kusonga mbele katika uwanja wa mapambano. 

Kwa sasa mapigano makali yanaripotiwa katika kijiji cha Bingi ambako waasi hao wanadhamiria kuyateka makao makuu ya wilaya ya Lubero. 
Ni miji midogo na muhimu ya Kanyabayonga pamoja na Kirumba iliyoangukia mikononi mwa waasi wa M23 wikendi hii iliyoisha. 

DW inaripoti kuwa waasi hao walisonga mbele na kuteka kijiji cha Kaseghe duru kutoka eneo hilo zimeeleza.

Kwa mjibu wa mashirika ya kiraia katika wilaya ya Lubero, mapigano makali yalizuka asubuhi ya leo jumatatu katika kijiji cha Bingi, kaskazini magharibi ya mji mdogo wa kibiashara wa Kirumba. 

Bingi ni kijiji muhimu kutokana na wingi wa madini ya dhahabu yanayopatikana kwenye ardhi ya kijiji hicho.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet