pmbet

Waasi wa Yemen waishambulia Israel.

Eric Buyanza

July 3, 2024
Share :

Kundi la waasi la wahouthi wa Yemeni wamethibitisha kushambuliana maeneo muhimu ya Taifa la Israel wakishirikiana na dola ya IS ya nchini Iraq.

Kupitia hotuba iliyorushwa nakituo kimoja cha runinga msemaji wa Houthi Yahya Saeed amesema oparesheni ya kijeshi imefanyika na wamehusika kwenye mashambulizi yaliyoikumba Israel bila  kuyataja maeneo hasa yaliyolengwa na kushambuliwa.

Waasi wa Houthi wanaoegemea upande wa Iran walianzisha mashambulizi ya ndege zisizo na rubani ( droni) na makombora katika njia muhimu ya baharini mnamo Novemba mwaka uliopita katika kile wanachosema ni kuonyesha mshikamano na wanamgambo wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Katika zaidi ya mashambulizi 70 waliyofanya wahouthi wamefanikiwa kuzamisha meli mbili, kuiteka moja na kuwaua mabaharia kadhaa.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet