Waasi wa Yemen washambulia meli ya mizigo
Eric Buyanza
June 10, 2024
Share :
Shambulizi la kombora lililofanywa na waasi wa Houthi wa Yemen, limelenga meli ya mizigo yenye bendera ya Antigua na Barbuda katika Ghuba ya Aden.
Kombora hilo lilipiga eneo la mbele la meli hiyo siku ya Jumamosi jioni, na kusababisha moto ambao ulizimwa na wafanyakazi wa meli hiyo.
Kombora la pili liliwakosa watu waliokuwemo kwenye boti ndogo karibu na eneo hilo lakini taarifa zinasema hakuna mtu aliyejeruhiwa.