pmbet

Waasi wateka kambi ya kijeshi nchini Mali

Eric Buyanza

May 2, 2026
Share :

Jeshi nchini Mali na washirika wake mamluki wa Urusi wanaripotiwa kuikimbia kambi muhimu ya kimkakati ya Tessalit na hivyo kambi kuangukia mikononi mwa waasi.

 

Afisa kutoka kundi hilo linalodai kujitenga la ukombozi wa Azawad FLA ameliambia shirika la AFP kwamba wanajeshi na mamluki waliokuwa kwenye kambi kuu ya Tessalit walisalimu amri kama walivyofanya katika mji wa Kidal, uliodhibitiwa na waasi hao mwishoni mwa wiki iliyopita. 

 

Chanzo cha kiusalama katika mji wa Gao kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba hakuna mapigano yaliyotokea na kwamba wanajeshi waliondoka hata kabla ya waasi hawajaingia.
 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet