pmbet

Waasi wateka wanajeshi 200 wa mali katika mji wa Kidal

Eric Buyanza

May 16, 2026
Share :

Nchini Mali, waasi wa Azawad Liberation Front, wanaotaka kujitawala Kaskazini mwa nchi hiyo, wanasema wanawashikilia wanajeshi zaidi ya 200 kama wafungwa wa kivita katika mji wa Kidal.

 

Waasi hao wameonesha mkanda wa video, ukiwaonesha wanajeshi hao waliovalia mavazi ya raia, na kueleza kuwa wengine walitoroka baada ya mji wa Kidal kuanguka mikononi mwao.
 

Aidha, waasi hao wamesema wanajeshi hao wa Mali wanaangaliwa vizuri, na wametoa wito kwa mashirika ya Kimataifa kuwatembelea ili kuthibitisha hilo.

 

Wakati hayo yakijiri, nalo jeshi la Mali limeendeleza mashambulizi ya angaa katika mji wa Kidal kuwalenga waasi hao, operesheni wanaosema itaendelea katika siku zijazo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet