Wabongo waumana ligi ya Uturuki, Opa akitamba mbele ya Diana
Sisti Herman
March 8, 2024
Share :
Nyota wa kimataifa wa Tanzania ambao wanacheza ligi kuu wanawake nchini Uturuki Diana Msewa anayecheza Amed Sk na Opah Clement anayecheza Besiktas wamekutana kwenye mchezo wa ligi ukishuhudia Besiktas ya Opah kuondoka na ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Amed ya Diana huku Opah akitupia bao la mwisho la timu yake.
Kabla ya kutimkia Uturuki Opah alipita Simba na Kigoma Sisters za Tanzania huku Diana akipita Ruvuma Queens.