Wabunge Kenya wapitisha Muswada wa Fedha 2024.
Joyce Shedrack
June 25, 2024
Share :
Wabunge Nchini Kenya wamepitisha Muswada wa Fedha wa mwaka 2024 kupitia kikao cha bunge kilichokuwa kinaendelea siku ya leo kabla ya waandamanaji kuvamia ndani ya bunge hilo.
Wabuge 195 walipiga kura ya ndio kupitisha muswada huo huku wabunge 106 wakipiga kura ya hapana kupinga kupitishwa kwa muswada huo.
Muswada huo utakuwa sheria rasmi baada ya kutiwa sahihi na Rais wa Nchi hiyo Dkt.William Ruto.
Maandamano ya kupinga Muswada huo yanaendelea katika maeneo mbalimbali Nchini Kenya huku waandamanaji wengine muda huu wakivamia ndani ya Bunge la Nchi hiyo na kufanya uharibifu mkubwa.