pmbet

Wabunge wapendekeza South Afrika kuitwa Azania

Sisti Herman

July 8, 2025
Share :

 

Chama cha Kisiasa cha African Transformation Movement (ATM) pamoja na vyama vingine vya siasa vinapanga kuwasiliana na bunge pamoja na Kamati ya Mapitio ya Katiba ili kubadilisha jina la Afrika Kusini na liitwe Jamhuri ya Azania, miongoni mwa mabadiliko mengine.

Chama hicho kinadai kuwa jina la sasa ni mabaki ya ukoloni na halioneshi utambulisho wa kweli wa watu wa Afrika Kusini.

Rais wa ATM na kiongozi wa bunge, Vuyo Zungula, alisema jina “Afrika Kusini” liliwekwa wakati wa ukoloni na lina uhusiano mkubwa na mifumo ya ukandamizaji iliyoanzishwa na Waingereza pamoja na Waafrika wa kizungu (Boers).

“Kabla ya mwaka 1652, hatukuwa Waafrika Kusini. Jina ‘Afrika Kusini’ lilitokana na Waingereza na Boers kuungana kuunda kile kilichoitwa Muungano wa Afrika Kusini, muundo uliobuniwa ili kuendeleza ukandamizaji dhidi ya watu wa asili,” alisema.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet