pmbet

Wabunge wazichapa live Bungeni

Sisti Herman

May 19, 2024
Share :

Vurugu zilizuka katika Bunge la Taiwan, Ijumaa asubuhi wakati wabunge walipokuwa wakijiandaa kujadili pendekezo la kuwapa wabunge mamlaka zaidi ya kusimamia na kuchunguza vitendo vya serikali.

Wanasiasa wa Taiwan walijikuta katika mapambano makali, wakishikana, kusukumiana, na kupigana ndani ya Bunge hilo, huku wakiwa na mvutano kuhusu mageuzi yaliyopendekezwa kwa chombo hicho cha kutunga sheria.

Wakati wa vurugu hizo, baadhi ya wabunge walizunguka kiti cha spika, wengine waliruka juu ya meza na kuwavuta wenzao hadi sakafuni.

Mapigano hayo yalizuiliwa mara kadhaa lakini yalirudi na kuendelea hadi mchana, hali iliyosababisha vurugu kubwa ndani ya bunge hilo la kisiwa hicho

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet