pmbet

WACHA WANIITE MPENDA PESA: Mimi nalinda mustakabali wa vizazi vyangu - Tijjani Reijnders

Eric Buyanza

September 23, 2026
Share :

Kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, Tijjani Reijnders, amewashangaza wengi kwa kuwa mkweli kupitiliza baada ya kukiri wazi kuwa maslahi makubwa ya kifedha ndiyo yaliyomfanya akubali kujiunga na klabu ya Al-Qadsiah ya Saudi Arabia akitokea Manchester City.
 

Reijnders mwenye umri wa miaka 28, alikamilisha uhamisho wa pauni milioni 51 kwenda Mashariki ya Kati mwezi uliopita baada ya kudumu kwa msimu mmoja pekee pale Etihad.

 

Katika mahojiano aliyoyafanya na vyombo vya habari, kiungo huyo hakutaka kuficha ukweli kuhusu uamuzi wake ulioshtua wengi.

 

Alipoulizwa kama uamuzi huo unamfanya aonekane kama mchezaji anaebabaikia fedha zaidi, Reijnders alijibu kwa ujasiri mkubwa:

 

"Mimi mroho wa pesa? Siwezi kubisha hilo. Siku zote unaweza kujifanya una maadili sana, lakini nadhani kila mtu angekubali ofa kama hii. Baada ya soka langu kwisha, sitaki kufanya kazi tena. Lakini hatua hii inaniruhusu kuweka sawa mustakabali wa vizazi vijavyo vya familia yangu. Kama uamuzi huu unamaanisha hadi wajukuu zangu wataishi kwa amani na usalama wa kifedha, kwanini nisiufanye?"

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet