Wachezaji bora Taifa Cup 2026
Sisti Herman
August 2, 2026
Share :

Nyota wa timu ya Songwe, Amini Mkosa, ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano (MVP) wa Taifa Cup 2026 baada ya kuonyesha kiwango bora katika kipindi chote cha mashindano.
Mkosa alikuwa miongoni mwa wachezaji walioleta mchango mkubwa kwa timu yake, akionyesha uwezo katika ulinzi na kusaidia timu yake kufanya vizuri kwenye michuano hiyo iliyofanyika Dodoma.
Nyota wa timu ya Dar es Salaam @manjinajmakarim ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano (MVP) wa Taifa Cup 2026 kwa upande wa wanawake baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika mashindano hayo.
Najma amekuwa na mchango mkubwa kwa timu ya Dar es Salaam kupitia uwezo wake wa kufunga, kutengeneza nafasi na kuiongoza timu yake kufanya vizuri, hali iliyomfanya kutambuliwa kama mchezaji bora wa mashindano.





