Wachezaji hawa tu ndio wenye uhakika wa nafasi msimu ujao
Eric Buyanza
May 3, 2024
Share :
Tajiri mpya wa klabu ya Manchester United Sir Jim Ratcliffe anaelezwa kutaka kukibadilisha kwa ukubwa kikosi cha sasa cha klabu hiyo huku ikielezwa wachezaji watatu pekee ndio wenye uhakika wa nafasi msimu ujao.
Wachezaji hao ni Kobbie Mainoo, Alejandro Garnacho, na Rasmus Hojlund.
Taarifa zinasema baada ya vikao kadhaa vilivyofanyika, viongozi wa klabu hiyo kubwa duniani wamebariki na wako tayari kwa mabadiliko makubwa ya kikosi.