pmbet

Wachezaji Ivory Coast wazawadiwa mamilioni ya pesa na nyumba za kifahari

Eric Buyanza

February 14, 2024
Share :

Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast na kocha wao Emerse Fae walizawadiwa pesa na nyumba za kifahari katika hafla iliyosimamiwa na Rais wa nchi hiyo Jumanne kusherekea ushindi wao katika fainali ya kombe la mataifa barani Afrika.
 

Tembo wa Ivory Coast waliishinda Nigeria katika fainali siku ya Jumapili na kunyakua taji hilo kwa mara ya tatu.
 

Kila mchezaji alipewa milioni 213 (kwa thamani ya kibongo) na nyumba ya kifahari yenye thamani sawa na pesa hizo.
 

Kocha Fae alipewa milioni 400 (kwa thamani ya kibongo) kwa kuongoza vizuri wachezaji wake baada ya kuchukua nafasi ya kocha mkuu aliyetimuliwa Jean Louis Gasset katikati ya mashindano kufuatia kipigo kibaya cha mabao 4-0 dhidi ya Equatorial Guinea.
 

“Mmeleta furaha kwa wanannchi wa Ivory Coast, hongera, hongera,” alisema Rais Alassane Ouattara.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet