pmbet

Wachezaji tisa wapewa 'Thank you' Barcelona

Eric Buyanza

July 1, 2024
Share :

Takriban wachezaji 9 wa Barcelona wameiaga klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mikataba yao Juni 30, 2024.

Wachezaji hao ni Cuéllar, Iker Goujon, Josep Cerdà, Saïdou Bah, Pau Víctor, Moha, Pelayo, Marc Vidal na Naim.

Taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya klabu hiyo ilisomeka hivi;

"Juni 30 ndio siku ya mwisho ya mkataba wa wachezaji wa Barca Atlètic; 
Pau Víctor, Moha, Pelayo, Marc Vidal, Naim, Cuéllar, Iker Goujon, Josep Cerdà na Saïdou Bah”

“Hii inamaanisha kwamba, wakati wao na klabu ya FC Barcelona umefikia mwisho,”

"Klabu inathamini kujitolea kwao na inawatakia kila la heri katika shughuli zao za baadaye za kimichezo na za kibinafsi" ilisema sehemu ya taarifa ya Barcelona. 



 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet