Wachezaji vijana wafute mitandao ya kijamii - Roberto De Zerbi
Eric Buyanza
November 7, 2026
Share :

Kocha mkuu wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi, amewataka wachezaji vijana wanaochipukia katika ulimwengu wa soka kufuta kabisa akaunti zao za mitandao ya kijamii na badala yake kuweka nguvu zao zote kwenye soka.
Kauli hiyo ya De Zerbi inakuja kama onyo kwa vipaji vichanga vinavyokabiliwa na changamoto ya kupoteza mwelekeo kutokana na umaarufu wa mtandaoni, jambo ambalo amesisitiza kuwa linaweza kuhatarisha maendeleo ya soka lao.
Akizungumza kuhusu umuhimu wa nidhamu na utulivu wa kiakili kwa wachezaji wa kisasa, kocha huyo raia wa Italia amebainisha kuwa mitandao ya kijamii imekuwa ikileta usumbufu mkubwa na shinikizo lisilo la lazima ambalo linaathiri viwango vya wachezaji uwanjani.
Tangu alipochukua mikoba ya kuinoa Spurs Machi 2026 na kuwaokoa kutoka kwenye janga la kushuka daraja msimu uliopita, De Zerbi amekuwa akisisitiza kujenga utamaduni wa nidhamu ya hali ya juu na utendaji kazi ndani ya kikosi hicho chenye maskani yake Kaskazini mwa London.





