Wachezaji wa Ireland wagoma kusalimiana na wenzao wa Israel
Eric Buyanza
September 28, 2026
Share :

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Ireland imegoma kusalimiana kwa kupepeana mikono na timu ya taifa ya Israel, ikiwa ni muendelezo wa mivutano ya kisiasa inayohamia viwanjani kutokana na vita vinavyoendelea huko Gaza.
Kabla ya mchezo huo uliochezwa Hungary na kumalizika kwa ushindi wa mabao 3-0 kwa Ireland, wachezaji wa Jamhuri ya Ireland na Israel hawakusalimiana kwa kupeana mikono. Aidha, wachezaji wa Ireland waliinamisha vichwa vyao wakati wimbo wa taifa wa Israel ukipigwa.
Nahodha wa Ireland, Dara O'Shea, na mwenzake wa Israel, Manor Solomon, pia hawakusalimiana kabla ya mechi, huku timu hizo mbili zikikosa kubadilishana bendera za kumbukumbu kama ilivyo kawaida.
Tangu droo ya Kundi B3 ilipofanyika mwezi Februari, mechi kati ya timu hizo zimezua mjadala kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Israel na Gaza.
Awali, baadhi ya wachezaji wa Ireland walikabiliwa na wito wa kujiondoa kwenye mashindano hayo, huku kampeni ya "Stop the Game", iliyoandaliwa na kundi la Irish Sport for Palestine, ikipata uungwaji mkono mkubwa katika wiki za hivi karibuni.





