Wachezaji wa Mali ni Vijeba - Kocha Afrika kusini
Sisti Herman
January 17, 2024
Share :
Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Afrika Kusini Hugo Broos baada ya kupoteza mchezo wa jana amesema kilichosababisha wapoteze mchezo ni penalty aliyoikosa Percy Tau dakika za mwanzo za mchezo.
Hugo pia ameweka wazi kuwa miili mikubwa ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Mali imesababisha wao kupoteza mchezo kwani hakutegemea kukutana na wachezaji wenye miili mikubwa vile.
“Sababu za kupoteza Mchezo dhidi ya Mali kwa upande wangu ni mbili tu, moja ni kitendo cha Percy Tau kukosa penati katika dakika za awali, angefunga ile penati ingeongeza ari kwetu na kupunguza moto wa mpinzani wetu”.
“Sababu ya pili ni wachezaji wa Mali kuwa na miili mikubwa, wengi wameshiba na wana nguvu pia, hatukujiandaa kwa hili”.
“Ukitazama wachezaji wangu walishindwa kuwahimilii kinguvu kwasababu katika wote niliowaanzisha hakuna anayewafikia”, Hugo Broos kocha wa Afrika Kusini.
Afrika Kusini jana ilipoteza 2-0 mbele ya timu ya Taifa ya Mali katika mchezo wa kwanza kwa kundi E.
Hadi hivi sasa kundi hilo linaongizwa na Mali yenye alama tatu [3] sawa na Namibia [3] tofauti ikiwa ni idadi ya magoli ya kufunga, Mali [2] na Namibia [1].