Wachezaji wa Mamelodi kuvuna bonasi ya Bilioni 15.
Joyce Shedrack
May 26, 2026
Share :
Klabu ya Mamelodi Sundowns imepanga kuwapa Wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi kiasi cha dola milioni 6 za Kimarekani ambazo ni takribani Bilioni 15 za Tanzania waliyolipwa na CAF kama zawadi ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwapa yote kikosi chao kama bonasi baada ya ubingwa huo.

Masandawana walitwaa ubingwa wa pili wa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili usiku baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 2-1 dhidi ya AS Far Rabat ya Morocco.
Viongozi wa Mamelodi wamepanga kuwapa wapambanaji wao mavuno yote ya michuano ya CAF ikiwa ni hatua hiyo inaonyesha falsafa ya muda mrefu ya klabu iliyoanzishwa wakati wa uongozi wa Patrice Motsepe na ambayo sasa inaendelezwa chini ya Mwenyekiti Tlhopie Motsepe.





