Wachezaji wangu walicheza vizuri - Ten Hag
Eric Buyanza
December 13, 2023
Share :
Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag mara baada ya kipigo cha goli 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya 6 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka kwa Bayern Munich, ametoa maoni yake huku akionyesha kuridhishwa na kiwango cha timu yake.
“Tulifanya makosa, lakini wachezaji wangu walicheza vizuri sana, jana hatukustahili kufungwa na Bayern Munich” Maneno ya Kocha Erik Ten Hag.
Baada ya matokeo hayo, Man Utd imemaliza nafasi ya mwisho kwenye kundi lenye timu kama Bayern, Galatasaray na Fc Copenhagen na kushindwa kufuzu hatua ya mtoano