Wachezaji watatu Yanga waaga, kujiunga na Simba
Joyce Shedrack
July 10, 2024
Share :
Wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza cha klabu ya Yanga Princess wameagana na klabu hiyo baada ya msimu wa ligi kuu wanawake kutamatika huku wakitajwa kuwa kwenye rada za watani zao klabu ya Simba Queens.
Siku mbili zilizopita kwa nyakati tofauti kiungo wa kati raia wa Nigeria Mary Saiki Atunike, Kiungo mshambuliaji raia wa Nigeria Precious Christopher na beki wa kushoto raia wa Kenya Wincate Kaari waliaga kuendelea kuitumikia Yanga huku siku ya jana Yanga ikiwaaga wote watatu kwa pamoja.
Chanzo kimoja ndani ya klabu ya Simba kimethibitisha kuwa wachezaji hao msimu ujao watacheza tena pamoja kwenye klabu hiyo ambao ni mabingwa wa ligi hiyo.