pmbet

Wachezaji wengi sio wazalendo kwasababu hawajazaliwa Cameroon - Etoo

Sisti Herman

January 22, 2024
Share :

Baada ya kupoteza mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya AFCON dhidi ya Senegal [3-1], Rais wa shirikisho la soka nchini Cameroon, Samuel Eto’o amewajia juu wachezaji wake kwa kukosa uzalendo kwa Taifa lao.

 

Eto’o ameweka wazi kuwa asilimia kubwa ya wachezaji wanaolitumikia Taifa hilo kwenye mashindano haya hawajazaliwa nchini Cameroon wala hawajawahi kucheza kwenye klabu yoyote ya Cameroon hivyo wamekosa uzalendo.

 

“Kaka zangu, nawaelewa, wengi wenu hamjazaliwa Cameroon na hamjawahi kuchezea hata klabu moja ya Cameroon”.

 

“Ushauri wa kocha wa Cameroon ni msaada mkubwa kwa wachezaji kuanzia mwanzo wa safari yake hadi mwisho, nyie ambao mmezaliwa huko mnahaki nyingi mbele ya viongozi”.

 

“Cameroon ilinifundisha mimi kuwa mimi ni mwanajeshi kwenye timu yangu ya Taifa, nitakufa na hii morali”.

 

“Cameroon inapitia udhalilishaji kwasababu upendo kwa Taifa hili sio wa asilimia 100, samahanini kwa kujizungumzia mimi”.

 

“Ningeweza kucheza mechi mbili kwa siku moja kwasababu ya upendo nilionao kwa Taifa hili zuri, nilifanya, Roger Milla alifanya na Francois Omam Biyick naye alifanya”.

 

“Hivi mnaamini kuwa Cameroon ilikuwa inatulipa zaidi ya klabu zetu ? Sio hata 1/10 tulichokuwa tunakipata sehemu nyingine”.

 

“Mnacheza sana kwa kujilinda mnaogopa nini ?, kufa kwaajili ya Taifa lako ni zaidi ya pesa zote za Dunia hii, Manga Onguene alivunjika mguu kwaajili ya Taifa hili, alikuwa bora zaidi yangu kwa kipindi kile, anaendelea kuliheshimu Taifa hili licha ya yote yale”.

 

“Kitu ambacho nakikumbuka kutoka kwenu Ijumaa hii, tumefanya makosa kuwaleta kucheza kwaajili ya bendera ya nchi, lakini baada ya AFCON mambo yatabadilika”.

 

“Tunaenda kufanya majaribio ya uzalendo kabla ya wachezaji wadogo wa Cameroon kucheza kwaajili ya Taifa lao, ni vizuri endeleeni kwenye mashindano”, Amesema Samuel Etoo, Rais wa Shirikisho la Soka Cameroon.

 

Timu ya Taifa ya Cameroon imesalia na mchezo mmoja pekee wa hatua ya makundi dhidi ya Gambia utakaopigwa Jumanne, January 23 majira ya saa mbili [20:00] usiku.

 

Cameroon wanapaswa kupata matokeo katika mchezo unaofuata ili wafikishe alama nne [4] ili waweze kufuzu hatua inayofuata kama best looser au mbele ya Guinea.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet