pmbet

Wachezaji Yanga wamtaka Sowa kuziba nafasi ya Mayele

Eric Buyanza

December 12, 2023
Share :

Baada ya Yanga kurejea Bongo ikitokea Ghana kwenye mchezo wake dhidi ya Medeama, inaelezwa kuna mastar wawili wa timu hiyo wameona kitu kutoka kwa mshambuliaji Jonathan Sowa wa Medeama na kuutaka uongozi wa Yanga kufanya kila linalowezekana kumshusha star kwenye kikosi hicho.
 

Mastar hao ni wachezaji wa zamani wa timu hiyo, Abeid Mzbna 'Tekero' na Sekilojo Chambua waliowahi kufanya vizuri na kikosi cha Yanga miaka ya nyuma.
 

Wakiongea na wanahabari wakongwe hao wamepaza sauti wakimtaka Engineer Hersi Said kufanya kila linalowezekana kumsajili haraka mshambuliaji huyo aliyewasumbua sana mabeki wa Yanga, ili kuwapunguzia stress katika mechi ambazo wamekuwa wakicheza za hivi karibuni.
 

Kwa mujibu wa wachezaji hao wa zamani wa klabu ya Yanga, Sowa anastahili kutua Jangwani kuziba nafasi ya Mayele kwani ni mtu sahihi sana.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet