Wachina watengeneza Betri inayokaa na chaji miaka 50 bila kuchajiwa
Eric Buyanza
January 25, 2024
Share :
Kampuni ya Kichina ya Betavolt hivi majuzi ilizindua betri yake aina ya BV 100 ambayo ni ndogo kuliko sarafu kwa ukubwa, lakini inaweza kutumika hadi miaka 50 bila kuchajiwa tena.
Betri hiyo ina ukubwa wa milimita 15 x 15 x 5, na huzalisha umeme wa microwati 100.
Kampuni hiyo imepanga kuanza kuzalisha kwa wingi betri hizo baadaye mwaka huu.
Wanasayansi wanasema hivi karibuni tunaweza kuona betri za simu ambazo hazihitaji kuchajiwa tena au vifaa kama ndege zisizo na rubani (drone) kuruka bila kutua.