pmbet

Wachungaji kurusha 'Shuhuda' za waumini bila idhini ni kosa kisheria

Eric Buyanza

March 24, 2025
Share :

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), imesema utaratibu wa wachungaji na watumishi kuweka hadharani taarifa binafsi za waumini wao katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa kigezo cha 'Ushuhuda' ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa mustakabali wa Maisha binafsi ya mhusika. 

Kauli hiyo ilitolewa jana Machi 23,2025 na Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Innocent Mungy wakati akitoa semina kuhusu siri za mtu na taarifa binafsi na umuhimu wa kuzihifadhi kwa waandishi wa habari mkoani Mwanza.

Vilevile, Mungy amesema kwa mujibu wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi namba 11 ya mwaka 2022 endapo mchungaji akichapisha taarifa binafsi za muumini bila idhini yake anayo haki ya kumshtaki na kulipwa fidia. 

“Muumini anayo haki ya kumshitaki mchungaji endapo taarifa za ushuhuda wake zimewekwa hadharani bila idhini yake na sisi kama tume tutashughulikia taratibu zote hadi anapata fidia hiyo kwani ni kinyume cha sheria kuweka taarifa binafsi za mtu,” anasema. 

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet