pmbet

Wafanya mtihani wa kujiunga na jeshi wakiwa na chupi tu

Eric Buyanza

July 11, 2026
Share :

Katika hali ya kushangaza mwaka 2015 lilitokea tukio nchini india ambalo kwa hakika lilivuta hisia za watu duniani kote, ni kwamba mamia ya vijana katika jimbo la Bihar waliokuwa wakitafuta nafasi ya kujiunga na jeshi la nchi hiyo walilazimishwa kufanya mtihani wakiwa wamevaa chupi tu, nia ikielezwa ni kuzuia udanganyifu kwenye mtihani huo.

 

Picha zilionyesha watahiniwa hao wakiwa wamekaa chini kwenye uwanja mkubwa huku wakiwa wameshikilia karatasi za mtihani.

"Tulipoingia tuliombwa kuvua nguo zote isipokuwa nguo za ndani. Hatukuwa na chaguo ila kufuata maelekezo ingawa ilionekana kuwa jambo la ajabu sana,” alisema mmoja wa watahiniwa alipoongea na gazeti la The Indian Express.

 

Bihar na sehemu nyingine nyingi za kaskazini mwa India zina sifa mbaya kwa udanganyifu wakati wa mitihani, itakumbukwa katika siku za nyuma serikali ya jimbo hilo iliaibika baada ya wazazi na marafiki kupigwa picha wakipanda kuta za shule ili kuwapa majibu ya mtihani wanafunzi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet