Wafoji saini ya Rais na kuiba dola milioni 6 Benki Kuu
Eric Buyanza
February 15, 2024
Share :
Nigeria imeanza kutafuta usaidizi wa Interpol ili kuwakamata watu watatu wanaodaiwa kuiba Dola Milioni 6.2, kutoka kwenye Benki kuu ya nchi hiyo, kwa kutumia sahihi ya kughushi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari.
Watu hao wanadaiwa kuwa ni washirika wa aliyekuwa Mkuu wa Benki Kuu ya Nigeria Godwin Emefiele, ambaye nae anakabiliwa na mashtaka 20, ikiwa ni pamoja na kupokea Dola Milioni 6.2 kinyume cha sheria.
Hata hivyo Bw.Emefiele amekana mashtaka yote, na sasa yuko nje kwa dhamana, huku Mamlaka nchini humo zikiamini kuwa washukiwa hao walikula njama na Bw.Emefiele, ili kutekeleza adhma yao.