pmbet

Wafungwa sasa ruksa kwenda kuzika ndugu zao

Eric Buyanza

February 24, 2024
Share :

Wafungwa na mahabusu nchini Kenya, sasa wataweza kuhudhuria maziko ya wanafamilia wao wa karibu, ikiwa hakuna sababu za msingi za kuwanyima haki ya kufanya hivyo.

Jaji Lawrence Mugambi amesema wafungwa pia wana haki ya kutendewa utu, hatua hii imekuja kufuatia kesi iliyofunguliwa na mwanahabari wa zamani Moses Dola, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela mwaka 2018 kwa madai ya kumuua mke wake .

Bwana Dola alifungua kesi hiyo baada ya kunyimwa kuhudhuria mazishi ya mama yake mzazi, hatua aliyoiita ukiukaji wa uhuru wa kimsingi na haki za wafungwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet