Wagombea kitoweo cha nyama ya mbwa kutoka Zambia
Eric Buyanza
February 21, 2024
Share :
Katika hali ya kushangaza zaidi ya mbwa 100 huingizwa nchini kongo (DRC) wakitokea Zambia kila mwezi kwa ajili ya kutumika kama kitoweo, limeandika gazeti la Zambia Observer.
Uchunguzi uliofanywa na shirika la kutetea haki za wanyama la nchini Zambia, umebaini hali hiyo ya kutisha na kusema bei sahihi ya nyama hiyo imeshindwa kujulikana kwa sababu biashara hiyo imekuwa ikifanyika kwa usiri.
Taarifa hizo za uchunguzi pia zimebaini kwamba nyama hiyo ya mbwa imekuwa na uhitaji mkubwa nchini Congo kiasi cha kuzua vurugu mpakani kwa wafanyabiashara wanaokuwa wakisubiria nyama hiyo kutoka upande wa Zambia.
Pia kwa upande wa Zambia inaelezwa kuwa wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakiuza 'nyama choma ya mbwa' wakiwaaminisha wateja kuwa ni nyama ya mbuzi, na wamekuwa wakifanya hivyo usiku hususan kwenye maeneo ya starehe kama mabaa.