Wagonjwa waliopona wagoma kuondoka Hospitali, kisa msosi
Eric Buyanza
February 10, 2024
Share :
Takriban watu 40 waliokuwa wamelazwa kama wagonjwa katika hospitali ya Mbagathi jijini Nairobi wamegoma kuondoka hospitalini hapo kurudi makwao hata baada ya kupona magonjwa yaliyokuwa yakiwasumbua.
Kwa mujibu wa kituo cha luninga cha Citzen uamuzi wa jamaa hao kugoma kuondoka hospitali unatokana na hali mbaya ya kiuchumi waliyonayo na hivyo kushindwa kumudu gharama za kujinunulia chakula endapo wangerudi majumbani kwao...hali iliyosababisha madaktari na wahudumu wa afya wenye huruma kuwapa chakula cha hospitali.
"Mtu ametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani lakini anaona afadhali abaki hospitalini kuliko kwenda. Wanasema hali ya nyumbani ni mbaya.....angalau hapa wana uhakika wa kupata chakula" alisema Seneta wa jiji la Nairobi aliyefanya ziara ya kushtukiza Hospitalini hapo.
Hata hivyo hali hiyo imeongeza changamoto za kifedha zinazoikabili hospitali hiyo.