Wahamiaji 90 wazama majini wakiwa kwenye safari ya kuzamia Ulaya
Eric Buyanza
July 6, 2024
Share :
Takriban wahamiaji 90 waliokuwa safarini kwenda barani Ulaya, wamepoteza maisha baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kuelekea ulaya kuzama kwenye pwani ya Mauritania.
Maafisa wa uokoaji Mauritania wanasema, wamefanikiwa kuopoa miili 89 baada ya boti hiyo kuzama kwenye Bahari ya Atlantic Pwani ya mji wa Ndiago.
Watu tisa tu akiwemo mtoto wa miaka mitano ndio waliopatikana wakiwa hai, lakini wengine 72 bado hawajapatikana. Ripoti zinasema kuwa boti iliyozama, ilikuwa na abiria 170 waliokuwa wametokea nchini Senegal na pamoja na Gambia.