pmbet

Wahamiaji harahu waliofukuzwa Marekani wapokelewa Sierra Leone

Eric Buyanza

May 21, 2026
Share :

Ndege ya kwanza iliyowabeba wahamiaji kutoka Afrika Magharibi waliofukuzwa nchini Marekani chini ya sera kali za uhamiaji za Rais Donald Trump iliwasili nchini Sierra Leone jana Jumatano.
 

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Sierra Leone Timothy Musa Kabba, wahamiaji 25 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Magharibi walikuwa ndani ya ndege hiyo iliyotua karibu na mji mkuu Freetown.

 

Polisi, wahudumu wa afya, maafisa wa serikali pamoja na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM walikuwepo kuwapokea wahamiaji hao katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa nchi hiyo.
 

Serikali ya Sierra Leone imekubali kupokea hadi wahamiaji 300 kwa mwaka wanaofukuzwa kutoka Marekani, lakini ni wale tu wanaotoka katika nchi wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS.
 

Waziri Kabba amesema baadhi ya wahamiaji hao wana vibali vya ukaazi vya Sierra Leone walivyovipata miaka mingi iliyopita, na kwamba wataruhusiwa kubaki nchini humo kwa siku 90 kabla ya kurejea katika mataifa yao ya asili.

 

Kwa mujibu wa nyaraka za wizara ya mambo ya nje zilizoonekana na AFP, Marekani imetoa dola milioni 1.5 kusaidia mpango huo kwa ajili ya gharama za kibinadamu na uendeshaji.

 

Sierra Leone sasa inaungana na mataifa mengine ya Afrika yaliyokubali kupokea wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani, yakiwemo Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ghana, Rwanda na Sudan Kusini.
 

Mashirika ya haki za binadamu yameendelea kukosoa makubaliano hayo, huku Human Rights Watch ikisema mikataba hiyo ya siri inakiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet