Wahitimu vyuo vikuu leteni mabadiliko kwenye jamii - Samia
Eric Buyanza
December 28, 2023
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuleta mabadiliko chanya katika jamii mara wanapohitimu masomo yao.
Ameyasema hayo leo mjini Zanzibar katika Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) na kueleza kuwa nimefarijika kuona wanawake wanazidi kuhamasika katika elimu.
“Nimepata faraja kuona asilimia 58 ya wahitimu leo ni wanawake,” amesema Rais Samia.