Wahouthi washambulia meli za biashara na moja ya kivita ya marekani
Eric Buyanza
June 17, 2024
Share :
Waasi wa Houthi wa Yemen walisema Jumapili kwamba wameshambulia meli mbili za kiraia, pamoja na moja ya kivita ya Marekani katika Bahari ya Sham na Bahari ya Arabia, katika juhudi zao za kuzorotesha safari za meli katika kile wanachosema ni kuwaunga mkono Wapalestina huko Gaza.
Katika taarifa yake, msemaji wa jeshi la Houthi, Yahya Saree, alisema wanamgambo hao walirusha makombora dhidi ya meli ya kivita ya Kimarekani iitwayo Captain Paris, na kutumia ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya meli ya kiraia iitwayo iitway Happy Condor.