pmbet

Waiomba serikali isihamasishe uzazi wa mpango, ili wazae kwa wingi

Eric Buyanza

February 29, 2024
Share :

Wakazi wa Kata za Ludende, Madilu na Milo zilizopo wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe wameomba serikali kupunguza kuhamasisha matumizi ya uzazi wa mpango ili waweze kuzaliana kwa wingi.
 

Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Afya, Malaria na Viashiria (Tanzania DHS-MIS 2022), ilionyesha wanawake walio kwenye ndoa na waliofikisha umri wa kuolewa (15-49) katika mikoa ya Njombe, Mbeya na Kilimanjaro ndiyo watumiaji zaidi wa njia zote za uzazi wa mpango kwa zaidi ya asilimia 50.
 

Aidha utafiti huo uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, unaonyesha wanawake kwenye mikoa ya Njombe wanatumia uzazi wa mapango kwa asilimia 64, Mbeya asilimia 58 na Kilimanjaro asilimia 63.
 

Hayo yameibuka katika mafunzo ya matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi mbalimbali wa wilaya na Halmashauri ya Ludewa.
 

Wamesema kwamba tangu serikali iwape elimu hiyo wananchi wameacha kuzaa na kusababisha vijiji vingi kuwa na mimba chache kwa mwaka na shule kukosa wanafunzi wa kutosha.
 

“Sisi hatuzai kwa sababu ya uzazi wa mpango ninaomba serikali ipunguze hata kidogo ili watu wazae sana itafika sehemu hatuna vijana kupitia uzazi wa mpango,” amesema.
 

Naye Izack Mhiche amesema kuwa ni vizuri hatua za haraka zikachukuliwa ikiwamo kupunguza elimu ili kusaidia wilaya hiyo kuwa na watu wengi.

Awali akiwasilisha mada katika mkutano huo mtakwimu kutoka NBS, Hellen Chuwa amesema kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022 Mkoa wa Njombe una watu 889,946 huku Wilaya ya Ludewa ikiwa na watu 151,361.
 

“Sio kwamba kwa vile mpo wachache hamtapata miradi hapana, takwimu zinarahisisha kujua ni wapi kitu kwa kiasi fulani kiende wapi,” amesema Chuwa.

Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga amesema kuwa suala la uchache wa watu linasababishwa na vitu vingi ikiwamo kuhamahama kwenda maeneo mengine kutafuta fursa.
 

“Kwa hiyo sasa ili Mkoa wa Njombe idadi ya watu iongezeke dawa yake ni kuwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi kuleta miradi mingine ije huku,” amesema Kamonga.

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet