pmbet

Waisraeli waandamana hadi nyumbani kwa Netanyahu kutaka vita isitishwe

Eric Buyanza

May 2, 2024
Share :

Raia wa Israel wamemiminika mitaani kuitaka serikali yao kusitisha 'umwagaji damu' na kufikia makubaliano na Hamas ili kuwarejesha mateka. 

Ndugu wa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na kundi la Hamas waliingia barabarani leo Alhamisi (Mei 2) kuishinikiza serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kundi hilo ili kurejeshwa kwa mateka wanaoshikiliwa.

Katika mji mkuu,Tel Aviv, waandamanaji waliweka vizuizi kwenye barabara kuu nyakati za asubuhi, huku wakipiga mayowe ya kutaka makubaliano ya haraka ili kukomeshwa kile walichosema ni 'umwagaji damu' na kuwarejesha mateka wote nyumbani. 

Wengine walikusanyika mbele ya nyumba ya Netanyahu kuwasilisha ujumbe wao. 

Mmoja wao alikuwa ni mama aliyebeba picha ya mtoto wake wa kiume, ambaye bado anashikiliwa mateka mikononi mwa Hamas.

Mama huyo alisema yeye na familia yake wako kwenye hali mbaya sana kama walivyo maelfu ya raia wengine wa Israel.
DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet