Waisraeli wanaopinga serikali yao waandamana nje ya Bunge
Eric Buyanza
April 1, 2024
Share :
Maelfu ya Waisraeli Jumapili ya jana walikusanyika nje ya jengo la Bunge mjini Jerusalem katika maandamano makubwa zaidi ya kuipinga serikali tangu nchi hiyo ilipoingia vitani mwezi Oktoba mwaka jana.
Waandamanaji hao wanaitaka serikali kufikia makubaliano ya kuwaachilia huru dazani za mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na kufanya uchaguzi wa mapema.