"Wakati Mamelodi wamemnunua mchezaji wa Bilioni 10, Yanga imemleta Guede Bure" - Gamondi
Sisti Herman
March 13, 2024
Share :
Kocha wa klabu ya Yanga Miguael Gamondi amesema wadau wa soka wasilinganishe ubora wa timu yake na wapinzani wao wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika Mamelodi Sundowns nje ya uwanja kwani mechi huchezwa ndani ya uwanja.
“Endapo utalinganisha bajeti ya Mamelodi Sundowns na yetu, bila shaka wao lazima uwape nafasi kubwa ya kushinda (Mamelodi). Mara ya mwisho walimnunua mchezaji mmoja kutoka Argentina kwa Dola za kimarekani milioni 4 (Bilioni 10 za Tanzania) na sisi tukamleta Guede na Okrah bila gharama yoyote (free agent). Hii ndio tofauti, lakini hiyo haina maana wakati mwamuzi anapopuliza filimbi ni 11 dhidi ya 11.” - Kocha Miguel Gamondi.
Gamondi amesema hayo akijibu swali kwenye mkutano na wanahabari kabla mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Geita Gold utakaochezwa kesho uwanja wa Azam Complex, Chamazi.