pmbet

Wakazi wakimbia, waasi wa M23 wakiusogelea mji wa Goma

Eric Buyanza

June 1, 2024
Share :

Wakazi wa mji wa Goma nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameanza kukimbia wakati ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakiwa wanaujongelea mji huo muhimu. 

Afisa mmoja wa serikali amenukuliwa akisema kuwa waasi wa M23 wanaukaribia mji wa Kanyabayonga uliopo kwenye njia inayoelekea katika mji wa Goma.

Kwa mujibu wa taarifa, mapigano yametokea kwenye eneo la Masisi karibu na mji wa Sake uliopo umbali wa kilometa 20 kutoka Goma.

Majeshi la serikali ya Kongo yamejaribu kuwarudisha nyuma waasi hao wa M23 wanaosemekana kuwa wameuzingira mji wa Goma ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet