pmbet

Wakenya 95 wasajiliwa kwenye jeshi la Urusi kupigana Ukraine

Eric Buyanza

February 19, 2026
Share :

Serikali nchini Kenya imebaini kuwa raia wake 95 wamesajiliwa kwenye jeshi la Urusi, kwenda kupigana nchini Ukraine. Takwimu hizi zimetolewa na Wizara ya Mambo ya nje, kwa mujibu wa Gazeti la Daily Nation.

 

Kati ya hao, 27 wamefanikiwa kurejea nyumbani, 33 wamesajiliwa hivi karibuni, wanane wameuawa na tisa hawajulikani waliko.

Vincent ni miongoni mwa Wakenya waliorejea nchini wiki iliyopita, baada ya kukwama katika mji wa Novgorod, Kaskazini Magharibu mwa Urusi, alifanikiwa kutoroka na baadhi ya rafiki zake, baada ya kutumwa kwenye mstari wa mbele nchini Ukraine.

 

Siku chache zilizopita, Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya, Musalia Mudavadi, alisema atazuru Moscow mwezi Machi, kulalamikia hatua ya Wakenya kujisajiliwa katika jeshi la Urusi.

 

Wachambuzi wa masuala ya usalama, wanasema Wakenya wanaojiunga na jeshi la Urusi kwenda kupigana Ukraine inasababishwa pakubwa na changamoto ya kupata ajira.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet