Wakili Mwabukusi ashinda kesi dhidi ya TLS
Sisti Herman
July 26, 2024
Share :
Mahakama Kuu ya Tanzania imetengua uamuzi wa Kamati ya Rufaa ya Chama Cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society) uliomwengua kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais wa chama hicho mmoja wa wagombea Wakili Boniphace Mwabukusi.
Uamuzi huo ambao umetolewa leo Julai 26, 2024 na Jaji Butamo Phillip unatoa hatima ya Mwabukusi katika kinyang’anyiro hicho.
Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanachama walioomba na kupitishwa na Kamati ya Uchaguzi kugombea nafasi ya urais wa TLS, lakini akapingwa kwenye kamati ya maadili ambayo ilimwengua.
Uchaguzi wa TLS unatarajiwa kufanyika Agosti 2, 2024 jijini Dodoma.