Wakina Aucho na Saido wajiweka kando Mapinduzi Cup.
Joyce Shedrack
January 2, 2025
Share :
Michuano ya mapinduzi Cup ni rasmi yatahusisha timu nne tu za Taifa na siyo sita baada ya Timu ya Taifa ya Uganda na Timu ya Taifa Burundi kujitoa kwenye mashindano hayo.
Timu zitakazoshiriki kwenye michuano hiyo ni Kenya (Harambee Stars) ,timu ya taifa ya BurkinafasoKilimanjaro Stars pamoja na wenyeji Zanzibar Heros.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kesho kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba kwa mchezo mmoja wa ufunguzi utakazozikutanisha Zanzibar Heros na Kilimanjaro Stars kuanzia saa 2:15 usiku.