Wakina mama walibeba waume zao mgongoni na kutokomea
Eric Buyanza
April 17, 2024
Share :
JE, WAJUA
Mwaka 1140, Mfalme Conrad III na majeshi yake waliuzungira mji wa Weinberg, kusini-magharibi mwa Ujerumani.
Kabla hajaliamuru jeshi lake kufanya shambulio la mwisho ili kuteketeza mji huo na vilivyomo, kwa huruma aliamua kuokoa maisha ya wanawake wote.
Akawapa masharti wanawake hao kuwa anawaruhusu kuondoka na kitu chochote kwenye mji huo ambacho wangeweza kukibeba migongoni mwao.
Cha kushtua ambacho Mfalme Conrad hakuamini, Wanawake hao waliacha mali zao zote na kutoka nje ya nyumba zao wakiwa wamebeba waume zao migongoni.
Conrad alipoona hivyo, alichoweza kufanya ni kucheka na kukubali huku akisema mfalme anapaswa kutimiza ahadi yake.