Wakuu wa mikoa fungeni TV muonyeshe mechi ya Serengeti Boys vs Senegal
Eric Buyanza
May 29, 2026
Share :

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe.Paul Makonda amewaomba Wakuu wa Mikoa yote nchini, kuweka Luninga kubwa kwenye maeneo ya wazi Jumanne ijayo wakati timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys itakapokuwa ikicheza fainali ya Afcon dhidi ya Senegal huko Morocco.
Makonda ameyasema hayo leo Bungeni, jijini Dodoma, wakati akichangia hoja ya kuipongeza Serengeti Boys, ambapo wabunge saba walichangia hoja hiyo iliyowasilishwa na Mbunge wa Bunda Mjini Mhe. Esther Bulaya.
Makonda Pia ameipongeza timu, benchi la ufundi na mlinda mlango Haji Alli, ambaye alizuia mikwaju miwili ya penati, katika ushindi wa Serengeti Boys wa penati 4-3 dhidi ya Misri kwenye mechi ya nusu fainali.





