Walibya 95 wakamatwa Mpumalanga kwenye kambi haramu ya kijeshi
Eric Buyanza
July 27, 2024
Share :
Polisi wa Afrika Kusini wametangaza kuwakamata Walibya 95 baada ya kuvamia eneo ambalo linaonekana kutumika kama kambi ya kijeshi.
Uvamizi huo ulifanyika mapema asubuhi ya jana Ijumaa karibu na mji wa White River, katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Mpumalanga, takriban kilometa 360 Mashariki mwa Johannesburg.
Imeelezwa kuwa eneo hilo lilitengwa awali kama kambi ya mafunzo kwa kampuni ya ulinzi, lakini pamebadilishwa na kuwa kama kambi haramu ya kijeshi," msemaji wa polisi Donald Mdhluli ameliambia shirika la habari la AFP.
Picha za televisheni za operesheni hiyo zinaonyesha kuwepo kwa polisi wengi nje ya kambi inayoshukiwa, ambayo ilikuwa na hema za kijani zenye mtindo wa kijeshi na mifuko ya mchanga.
Waziri wa ulinzi na usalama wa Mpumalanga, Jackie Macie, alisema wanaume hao waliingia nchini humo mwezi April na kudai wanapitia mafunzo kwa ajili ya kuwa walinzi.
Kuna wasiwasi kuwa nchi hiyo inaweza ikawa kituo cha ufadhili wa wanajihadi barani Afrika.