Walidanganywa wakiondoka 'Konde Gang' watafanikiwa, lakini imekuwa ndivyo sivyo!
Eric Buyanza
February 24, 2024
Share :
CEO wa Konde Gang ametangaza kusaini wasanii wawili wapya mwaka huu, huku akiwasikitikia wale walioondoka kwenye lebo hiyo kwa kudanganywa kuwa watapata mafanikio zaidi wakiwa nje, lakini imekuwa ndivyo sivyo.
Harmonize anasema ilifika wakati alikata tamaa kabisa kusupport wasanii chipukizi.
"Nimekaa Hapa Nawatazama Wale Waliofanikiwa Kuwatia Ujinga Wasanii Wengine Ambao Walikuwa @kondegang Na Kuwaaminisha Watafanikiwa Zaidii. Hata Mimi wakati Mwingine Ilinibidi Niamini Hivyo Ndiomaana Kwa Moyo Mkunjufu Nilizibariki Safari Zaoo!!! Ila Chakusikitisha IMEKUWA SIVYO NDIVYO !! 😢 Busara Unyenyekevu Uvumilivu Nibaadhi Ya Vitu Vinamfanya CHINGA Awe Hapa Leo!!!! PROUD OF YOU BROTHER ushauri Wako Naufanyia Kaziii Ingawa Nilikaribia Kukata Tamaa Kabisa Kuwa Support Wasanii Wengine Ila MANENO YAKO YAMENIPA NGUVU UPYA!!!! 2 MEMBERS @kondegang HUU MWAKA !!! 2024
👸 & 🤴Mtag Msaniii Unaemuona MKALI ILA HAJAPATA Nafasi!"